HabariNews

LALA SALAMA SHUJAA! Ruto aomboleza kifo shujaa Muthoni Wa Kirima

Rais William Ruto Jumanne Septemba 5, 2023 aliongoza taifa kuomboleza kifo cha mpiganaji wa uhuru Muthoni wa Kirima. Muthoni anasemekana kuaga dunia Jumatatu usiku Septemba 5, 2023.

 “Nimehuzunishwa sana na kuaga kwa Field Marshall Muthoni Kirima, mtu mwenye ushawishi mkubwa aliyepigania uhuru wetu,” Ruto alisema.

 Mwenda zake alihudumu kama msaidizi binafsi wa Dedan Kimathi katika mapambano ya ukombozi. Akituma risala zake za rambirambi, Ruto alimsifu Muthoni kama mwanamke jasiri, mchapakazi aliyeipenda familia yake akimtaja kama kjasiri alijitoa mstari wa mbele kuipigania jamii pamoja na nchi yake.

 “Tunaheshimu mchango wake wa kishujaa kwa uhuru na maendeleo ya nchi yetu na tunamwomba Mungu aipe familia nguvu katika wakati huu mgumu. Pumzika kwa Amani, Shujaa wetu,” Ruto aliongezea.

Vili vili Naibu Rais Rigathi Gachagua alimkumbuka Muthoni kama shujaa aliyeongoza jamii ya Agikuyu katika vita vya kupigania uhuru na kuombea faraja familia yake.

Tunabaki kuwa na deni kubwa kwa mashujaa hawa kwa Sadaka ya kuikomboa nchi yetu. Mungu ampumzishe kwa amani ya Milele na awape nguvu familia yake kubeba msiba huo,” alisema.

Mwendazake atakumbukwa mnamo aprili 2022 alinyoa nywele zake alizokua nazo tangu mwaka 1952,  zilizonyolewa na mama Ngina Kenyatta.

BY EDITORIAL DESK