Uncategorized

Vita dhidi ya Unyakuzi wa Ardhi Mombasa Vyasheheni Wakaazi Wakihamasishwa kupata Hati Miliki

Mombasa ikiongoza kwa visa vya uporaji na unyakuzi wardhi, Kuna haja kwa wakaazi katika kaunti hio  kuhamasishwa kuhusu jinsi ya kupata hatimiliki za ardhi zao.

Afisa msimamizi katika idara ya ardhi, makao na masuala ya mazingira katika shirika la Haki Yetu John Paul Obonyo aliunga mkono kauli hii akisema kuwa hatua hiyo itasadia pakubwa kupunguza kesi nyingi za ardhi.

Obonyo alidai kuwa takribani asilimia 45 ya kesi zilizoko mahakamani zinahusu utata wa umiliki wa ardhi.

“Jambo lakwanza ni kuweza kuhamasisha jamii kujua ardhi hio ni ya aina gani, waweze kufanya utafiti, na kufanya sachi twahitaji nini, kwanza lazima ujue ardhi hio iko na plot namba, pili ardhi hii iko na CR namba / coast registry ama namba ya faili, tatu uweze kuwa na KRA pin, nne uweze kuwa na copi ya kitambulisho chako na mwisho uweze kuwa na copi ya hati miliki yako”. Paul alisisitiza.

Kulingana na Obonyo shirika hilo linashirikiana na serikali kuhamasisha jamii kuhusu haki zao za kumiliki ardhi ili kuepukana na dhulma zinazoambatana na suala hilo.

“wakati unafanya masuala ya ardhi ,letu kama mashirika ni kufanya utafiti , pili nikuorganize Jamii zetu ili waweze kujua ni vipi wanaweza kushiriki kushirikiana na washikadau mbali mbali, tatu pia ni kuweza kuhamasisha serikali,” alisema

Haya yanajiri siku moja baada ya jamii ya Dzitengezere katika eneo bunge la Nyali Kaskazini kupata hatimiliki ya ardhi ya ekari 5.9 ambayo wamekuwa wakizozania mahakamani kwa muda mrefu.

BY EDITORIAL DESK