HabariNewsUncategorized

Tamu Chungu ya Chungwa! wabunge 5 Wakibanduliwa Nje ya ODM

Kamati Kuu ya chama cha ODM (NEC) kimetangaza uamuzi wa kuwatimua wanachama watano.

Wabunge waliotimuliwa ni Elisha Odhiambo kutoka eneo bunge la Gem, mbunge wa Bondo Gideon Ochanda, Felix Odiwuor maarufu ‘Jalang’o’ wa Lang’ata, Caroli Omondi wa Suba Kusini pamoja na Seneta wa Kisumu Tom Ojienda.

Katika taarifa  kwa vyombo vya habari Jumatano tarehe 6 Septemba, baada ya kikao kilichoongozwa na kinara wa chama Raila Odinga na Mwenyekiti wa kitaifa John Mbadi, kamati hio ilisema kuwa uamuzi wa kuwatimua wanachama hao ulifikiwa kufuatia ripoti ya kamati ya nidhamu iliyokuwa ikichunguza mienendo ya baadhi ya wanachama.

Chama hicho aidha kimewatoza faini mbunge wa Rongo Paul Oduor na Mark Nyamita kutoka eneo bunge la Uriri, kila mmoja akitozwa shilingi milioni moja kwa ukosefu wa nidhamu.

Hata hivyo viongozi hao wanatarajiwa toa faini hio ndani ya siku sitini.