HabariNews

AFUENI, NACADA Yakataa uwepo wa dawa ya Fentanly

Mamlaka ya kudhibiti utumizi wa mihadarati na unywaji wa pombe nchini NACADA imekanusha kuwepo kwa dawa mpya aina ya Fentanly.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa baadhi ya waraibu wanachanganya heroini na dawa nyingine za madukani.

Kulingana na mkurugenzi wa mamlaka hio prof John Muteti, dalili za uzezeta miongoni mwa waraibu huenda zikatokana na uchanganyaji wa dawa zaidi ya moja hususan dawa zinazotolewa kulingana na maagizo ya daktari ili kusaidia kuongeza makali ya heroini ambayo imethibitishwa kupungua.

“kutokana na uchunguzi tuliofanya tumepata kuwa dalili ya kizezeta miongoni mwa waraibu huenda ikawa ni utumizi wa heroini kupita kiasi ama mchanganyiko wa dawa za zinazoagizwa na daktari na heroini.” Alisema

NACADA ilisema kuwa uvumbuzi wa dawa ya aina ya Xylazine unamadhara makubwa kwa watumizi ikisema kuwa inavunja makali dawa ya Naloxone inayotumika kudhibiti utumizi wa dawa kupita kiasi.

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo cha urekebishaji tabia kwa waraibu cha Reachout, Taib Abdulrahaman mikakati imewekwa ili kudhibiti maduka ya kuuza dawa mitaani na kuhakikisha wanapata ripoti kuhusiana na dawa hiyo akidokeza kuwa uchunguzi huo haujaonyesha waraibu wa dawa hiyo. Hali hii aliitaja kama afueni iliyoleta matumaini kwa kukosekana kwa dawa hiyo.

” Kuna mikakati ambayo imewekwa kuweza kuangalia ni vipi kutakuwa na mafatilizo kwenye maduka ya dawa kuweza kujua na sisi wenyewe ambao tuko mashinani kuweza kupeana ripoti halisi ili kufanyika usawa katika kupatika kwa hizi dawa.” Alisema Taib

Mamalaka hiyo hatahivyo ilitoa wito kwa jamii kuwa macho na iwapo watapata ripoti yoyote kuhusiana na dawa hiyo wajulishe asasi husika haraka iwezekanavyo ili kuepukana na madhara yanayaoiandama jamii.

Itakumbukwa kuwa mwezi Agosti 2023, mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuhusu kuwepo kwa dawa mpya ambayo ilikuwa imesambazwa na kuomba muda wa wiki mbili ili kufanya uchunguzi wa aina ya dawa hiyo.

BY EDITORIAL DESK