HabariNews

Watoto wenye umri wa miaka 10 wahusishwa na Visa vya Uhalifu Kilifi

watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 8 hadi 11 wamehusishwa pakubwa na visa vya uhalifu vilivyometajwa kuongoza kaunti ya Kilifi. Uhalifu  umetajwa kuongezeka kufuatia wengi wa watoto kukosa kwenda shule licha ya agizo la serikali kutaka kila mtoto aliyefikisha umri wa kwenda shule kuwa shuleni.

Kwa mujibu wa Khamisi Ali ofisa wa usalama nyanjani, ongezeko la visa hivyo ni kutokana na familia nyingi kukosa uwezo wakuwalipia watoto wao karo, pamoja na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.

“Ripoti ambazo nazipokea nyingi za uwizi ni za watoto wadogo miaka 10, 9 miaka 8 ambao ndio wanakua ni waizi, na kitu ambacho kinasababisha Yule mtoto zaidi ya kwamba ataendelea kua mwizi na takua jambazi mkubwa ikiwa serikali haitajaribu kuangalia , ni sababu Yule mtoto hata wakati anaposhikwa akifikishwa polisi station anaambiwa bado ni mtoto. Ukija ukiangalia uhalifu mwingi unaofanywa saii haufanywi na watu wakubwa” alisema

Kulingana na Kibibi Ali, mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto katika shirika la Kilifi Mum’s, wazazi kutelekeza majukumu yao kumechangia pakubwa kushuhudiwa kwa visa hivyo, watoto wakiishia kuiba ili kujinunulia bidhaa za uraibu akitolea mfano “Mugukaa”.

Kibibi alitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kilifi kupiga marufuku uuzaji wa “Mugukaa” huku akiwataka wazazi kuwa waangalifu na aina ya malezi wanayotoa kwa wanao ili kuepuka kuchangia kupotoka kwa maadili ya kizazi kijacho.

“serikali ya kilifi kaunti na serikali kuu zote zikiwa ndani ya Kilifi ziende zikapige marufuku uuzaji wa Mugokaa,na wazazzi wasipeane watoto pesa kila siku kuwafudisha pesa siku watoto wakikosa pesa wanaiba ili tu wapatepesa katika mifuko yao” alisema Kibibi.

BY ERICKSON KADZEHA.