Uncategorized

Siku ya Makazi Duniani, Mombasa kujenga makazi ya bei nafuu

Kenya imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya Makazi duniani, huku mataifa mbalimbali yakitakiwa kusaidia ukuaji wa miji.

Akiongea katika hafla ya kuadhimisha siku hio, mnamo Oktoba 2, Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir alibaini kuwa kaunti hiyo imeweka mikakati kuhakikisha kuwa wakazi wanapata makazi bora katika miji.

“Asilimia kadhaa katika zile nyumba zitakuwa pale lazima tuweke tenant purchase scheme kumaanisha kuwa mtu akilipa analipa kama kodi lakini baada ya miaka nyumba inakuwa ni yake.” Alisema.

Kulingana na gavana Nassir makazi yote katika miji yatakuwa ya viwango mbalimbali kulingana na uwezo tofauti tofauti wa kifedha kwa wakenya na watu wataishi kulingana na mapato yao.

“Sisi tukiweka zile nyumba kuna wale matajiri kama ataweza atanunua ile nyumba na yule ambao ako na ajira utajiri wake ni wastani atanunua kwa upande ule, inamaamisha there is high end affordable watu wa Mombasa wanufaike,” alisema Nassir.

BY MJOMBA RASHID