HabariNews

Serikali Yaagiza kuhamisha Polisi waliohudumu zaidi ya miaka 3 katika kituo kimoja

Serikali imeagiza kuhamishwa mara moja kwa maafisa wa polisi waliohudumu katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitatu.

Kindiki aliitaka tume ya huduma za polisi kulifanyia kazi pendekezo hilo huku akitoa makataa ya siku 60 kwa suala hilo kutekelezwa.

Vilevile alitoa onyo kwa afisa atakayekaidi agizo hilo kusitishwa mshahara wake

Kulingana na Kindiki sera hiyo ni mojawapo ya mapendekezo yaliyotolewa na jopokazi linaloshughulikia mageuzi ya idara ya polisi inayoongozwa na jaji mkuu mstaafu David Maraga.

Hali kadhalika waziri huyo alitoa amri kwa maafisa wanaohudumu katika vitengo maalum kutopitisha mwaka mmoja katika kituo kimoja wanapokabidhiwa majukumu maalum.

Sera hiyo hata hivyo ilitiliwa mkazo na Rais William Ruto ambaye alinukunuliwa akilitaja suala hilo kama mojawapo ya vigezo vya kupandishwa vyeo kwa maafisa wa usalama humu nchini.

BY EDITORIAL DESK