HabariNewsSiasa

Jiungeni na chama cha PAA, ili Pwani iwe na ushawishi Serikalini

Ili kuwa na usemi na ushawishi mkuu serikalini kuna haja kubwa viongozi wa ukanda wa Pwani sasa kujiunga na chama cha kisiasa cha PAA.

Ni kauli yake Katibu mkuu wa chama cha PAA Lucas Maitha ambaye aliwasihi viongozi kutoka ukanda wa pwani kukumbatia chama hicho na kufaniklisha maendeleo ukanda huo.

Akizungumza katika kipindi cha gumzo pevu Katibu huyo aliwataka  viongozi wa pwani kuwa na msemaji wao kama maeneo mengine, huku kuwepo kwa changamoto za kutoamiana kati ya viongozi hao swala analodai kutatuliwa na chama cha PAA.

Sisi Wapwani tumekuwa hatuaminiani, safari ili tuaminiane tumpishe mmoja wetu mbele awakilishe masuala yetu mbele. Tuunge mkono PAA viongozi wajiunge ili tuwe na sauti. Uongozi unajitokeza tukiungana kuonyesha ukomavu,” alisema.

Mbunge huyo wa zamani kadhalika alipongeza hatua ya rais William Ruto kukubali ombi lao la kutaka baadhi ya viongozi kutoka ukanda wa pwani kuteuliwa kuongeza raslimali za kipwani akitoa mfano katika wizara ya uchumi samawati.

Tulimwambia Rais sisi hapa hatuna majani chai wala kahawa raslimali yetu kubwa ni Bahari, tutanufaika vipi? Tukamwambia Bahari ina utajiri mkubwa, akachukua mtoto wetu ambaye amepewa mamlaka kusimamia hiyo rasilimali na niwetu sisi ambaye ni Salim Mvurya endapo atafaulu basi atakuwa amesadia watu wake na akishindwa basi ataumiza watu wake mwenyewe,sasa tutamlaumu Rais Ruto na wapi ?” alisema.

Hata hivyo Maitha ameongeza kuwa chama cha PAA kwa sasa kinanuia kupata viti vingi vya kisiasa katika uchaguzi wa 2017 na kutaka wapwani kuungana na chama hicho.

BY DAVID OTIENO