HabariNews

Idara ya Afya Mombasa Yatoa Tahadhari ya Mlipuko wa Ugonjwa wa Macho ‘Red Eyes’

Idara ya afya kaunti ya Mombasa imeutaka usimamizi wa shule kuwa wangalifu dhidhi ya wanafunzi kuhusu maradhi ya macho ijulikanayo kama macho mekundu (RED EYE DISEASE).

Afisa wa afya Dkt Salma Swale amerai walimu katika shule zote katika meneo bunge yote kuhakikisha kwamba wameweka mikakati ya kuzuzia maradhi hayo.

Miongoni mwa mikakti hiyo ni kuhimiza wanafunzi kudumisha usafi, kunawa mikono mara kwa mara, kutogusa macho yao kwa mikono, kufunika midomo wanapokohoa au kuchemua ili kudhibiti maambukizi.

Aidha DKt Salma amewahimiza walimu kuwapeleka wanafunzi katika vituo vya afya iwapo wataonekana na dalili za ugonjw ahuo ikiwemo kuvimba kw macho,kujikuna macho hali isiyo kawaida.

Kupitia kwa taarifa kwa vyombo vya habari hapo jana idara ya afya ya kaunti hiyo imethibitisha visa kadhaa kvya ugonjwa huo katika baadhi ya vituo vya afya unaoweza kusababishwa na kusambaa kwa viiini tofauti kutoka kwa sehemu hadi nyingine.

BY NEWSDESK