HabariNews

Ombi la Makenzie latupiliwa Mbali na mahakama

Mshukiwa mmoja kati ya 31 wanaohusishwa na mauaji ya Shakahola amekosa kusomewa mashtaka baada ya idara ya mashtaka kusema uchunguzi wa akili aliofanyiwa ulionyesha hawezi kujibu mashtaka.

Evans Sirya Sasa atasalia korokoroni Kwa kipindi Cha mwezi mmoja kabla ya kufanyiwa vipimo na kuwasilishwa mahakamani.

Mahakama hiyo imeambiwa Sirya Kwa Sasa anaugua na kuwa huenda idara ya mahakama ikamshtaki punde tu atakapo kuwa salama kujibu mashtaka.

Awali mawakili wa washukiwa hao wakiongozwa na Wicliff Makasembo walipinga kusomewa mashtaka Kwa washukiwa hao wakisema ni kinyume cha sheria kufuatia wingi wa mashtaka.

Hata hivyo Jaji Mugure Thande amelipinga ombi hilo na kuamuru zoezi hilo kuendelea akisema mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria kuzuia zoezi hilo.

Wakati huo huo Mshukiwa mkuu katika mashtaka hayo mhubiri tata Paul Mackenzie aliitaka mahakama kuwasomea mashtaka kila mshukiwa kivyake ili waweze kuchukua maamuzi ya kibinafsi badala ya kuchukua Kwa pamoja.

Jaji Thande vile vile alilitupilia mbali ombi la Mackenzie na kuamuru washukiwa wote kusomewa mashtaka yote 191 Kwa pamoja.

BY JOSEPH YERI