HabariLifestyleMombasa

Polisi Wamkamata Kiongozi wa Genge Linalohangaisha Wakazi wa Mombasa

Idara ya Polisi kaunti ya Mombasa imemkamata kiongozi wa genge moja hatari la uhalifu linalohangaisha wakazi wa Kibokoni maeneo na mengi ya mji wa Mombasa.

Kwa mujibu wa ripoti za polisi Abdulkadir Mohammed ambaye ni kiongozi wa genge linalojiita Kibokoni Panga Boys alinaswa na maafisa wa polisi wa Central akihudhuria mechi ya mpira eneo la Kibokoni baada ya maafisa kupokea taarifa za kijasusi.

Mshukiwa huyo alipatikana na panga ndani ya suruali yake aliyokuwa amevaa ishara kuwa alikuwa sehemu ya genge hilo linalohangaisha usalama kwa kuwaibia na kuwajeruhi watu mjini Mombasa.

Kukamatwa kwa Abdulkadir kunajiri miezi kadhaa baada ya mshukiwa huyo akiwa pamoja na kakaye Hassan Noor kunaswa na kamera wakiwatishia na kuwahangaisha wakazi wa Kibokoni mjini Mombasa.

Awali wawili hao walinaswa mamo wmezi Oktoba mwaka 2023 wakiwashambuliwa wakazi eneo la Mji wa Kale ambapo mtu mmoja aliachwa akiuguza majeraha mabaya ya mapanga.

 

BY NEWS DESK