AfyaMakala

Wakaazi waomba zahanati kufungulia Msitu wa Boni

Jamii ya waboni kaunti ya Lamu sasa inaomba serikali kufungua zahanati na vituo vingine vya afya vilivyofungwa katika vijiji 6 miaka 7 iliyopita kutokana na mashambulizi ya kigaidi kutoka kundi la Alshabab. 

Zahanati za MilimaniMararaniBasubaKiangwe na Pandanguo zilivamiwa, kuporwa na hata kuteketezwa moto wa magaidi wa alshabab waliokuwa wakivamia maeneo hayo kati ya mwaka 2014 na 2017 hatua iliyosababisha wahudumu wa afya kuhama maeneo hayo,

Jamii hiyo inayoishi ndani ya msitu wa Boni ambako Magaidi hao wamekuwa wakijificha, wanalaumu serikali wakidai imewatelekeza kwa kutoangazia swala la afya.

Mwakilishi wadi ya Basuba Deko Barissa anataka serikali kufungua vituo hivyo vya afya kama ilivyofanya kwa vituo vya elimu vilivyofungwa wakati huo kutokana na sababu za utovu wa kiusalama.

Shule zote sita zilifunguliwa wiki mbili zilizopita na walimu mkusafirishwa kwa ndege hadi maeneo yao ya kufanyia kazi.

Kwa sasa zahanati za Kiangwe na Pandanguo zinahudumu japo zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wahudumu, dawa za matibabu na miundo msingi duni.

Comment here