Siasa

MWASHETANI ASISITIZA KUWANIA UGAVANA KWALE

Mbunge wa Lungalunga kaunti ya Kwale Khatib Mwashetani amesisitiza kuwania kiti cha ugavana wa Kwale katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha za makundi ya wanawake eneo la Kombani, Mwashetani amewataka wakaazi kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania ugavana.

Kiongozi huyo amesema kuwa analenga kuimarisha makundi ya maendeleo ya wanawake endapo atachaguliwa kuwa gavana wa kaunti hiyo.

Hata hivyo, Mwashetani amemkosoa gavana wa Kwale Salim Mvurya na naibu wake Fatuma Achani kwa madai ya kutoa fedha kidogo za makundi hayo.

Mbunge huyo aidha ameahidi kuendeleza mpango wa basari wa kaunti na miradi ya maendeleo ya serikali ya kaunti hiyo.

Comment here