Habari

Aliyekuwa Mbunge wa Garsen Ibrahim Sane anataka Viongozi wa kaunti na wa serikali kuu kusuhulisha migogoro.

Aliyekuwa Mbunge wa Garsen Ibrahim Sane anataka Viongozi wa kaunti na wale wa serikali kuu kuingilia kati na kusuhulisha migogoro iwapo itatokea eneo hilo bila kupendelea rangi, dini wala kabila.

Sane amewataka wakaazi wa kaunti ya Tana River kutojihusisha na malumbano na kuishi kwa amani.
Amewataka wakaazi hao kuripoti visa vyovyote vya ukosefu wa usalama kwa idara husika tofauti na kuchukua sheria mikononi mwao.

Wakati uo huo Sane amelaani tukio la hivi majuzi ambapo wakaazi wa Bandi na wale wa bula tawfiq walizozania kipande cha ardhi eneo la minjila na kulazimu maafisa wa usalama kuingilia kati.

Na: Guracho Salad.

Comment here