Habari

Mwanamme mmoja amepatikana ameuawa eneo la Likoni,Mombasa.

Mwanamme mmoja amepatikana ameuawa katika nyumba moja ambayo ilikuwa ikiendelea kujengwa katika mtaa wa Mrima Likoni hapa Mombasa.

Mama wa mtaa eneo hilo Fatma Nuri amesema wamepata mwili huo ukiwa na majeraha baada ya kujulishwa na majirani kuhusu kisa hicho.

Nuri amesema kijana huya emekuwa akifahamika kama “Masai” na alikuwa mlinzi wa nyumba hiyo inayoendelea kujengwa.

Aliyetekeleza unyama huo anadaiwa kutochukua chochote katika nyumba hiyo.
Polisi wamewasili eneo la tukio kuchukua mwili na kuupeleka katika hifadhi ya maita katika hospitali kuu ya kanda ya pwani huku wakianzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

Na:Joseph Jira.

Comment here