Gavana wa kaunti ya Machakos Dkt Alfred Mutua amewataka viongozi wa kisiasa kukoma kuhujumu juhudi za kuimarisha amani nchini.
Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari Mutua amewakemea viongozi wanaodaiwa kumtaka kinara wa upinzani nchini Raila Odinga kujiondoa kwenye makubaliano hayo.
Mutua anasema taifa hili halingeimarika kiuchumi na kisiasa endapo Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi huyo wa upinzani Raila Odinga hawangeweka makubaliano hayo.
Wakati uohuo kiongozi huyo wa chama cha Maendeleo Chap Chap amesema wapo viongozi walioshindwa kusambaza maendeleo kwa jamii wakiishia kutumia jamii zao maskini kujinufaisha wenyewe.
Amewashauri viongozi hao kukoma kutumia njia za mkato wanapotafuta nyadhifa mbali mbali za uongozi.
Haya yanajiri huku baadhi ya magavana ukanda wa pwani wakimshauri Raila Odinga kuiacha handisheki.