HabariSiasa

Mwakilishi wadi wa Tsimba Golini alaumiwa kwa ubaguzi wa miradi…

Baadhi ya Wakaazi wa wadi ya Tsimba golini katika kijiji cha Mazumalume kaunti ya Kwale wanamlaumu mwakilishi wadi wao Swaleh Simba kwa kubagua baadhi ya vijiji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakizungumza wakati wa kutoa maoni ya kutathmini  bajeti katika miradi ya maendeleo,  wakaazi hao wakiongozwa na Nyamawi Mwandia wanasema kwamba mjumbe  huyo anahusika katika kupeleka miradi mingi kwenye kijiji kimoja cha Mbuguni ambako anatoka licha ya wadi hiyo kuwa na vijiji vinne.

Mwandia amedokeza kwamba mwaka wa fedha wa 2020/2021 walipendekeza miradi kadhaa katika wadi hiyo ambapo kijiji cha Kundutsi na Mazumalume walipata miradi kidogo sana.

Haya yanajiri huku wakaazi hao wakitaka miradi ya mwaka 2021/2022  navyo vijiji vya Kundutsi na Mazumalume kupata miradi zaidi sawia na vijiji vya golini na Mbuguni.

By NewsDesk