AfyaHabari

Wahudumu wa afya Kwale waonywa kuuza dawa kinyume cha sheria…

Wizara ya afya kaunti ya Kwale imewaonya vikali wahudumu wa afya wanaouza dawa kinyume na sheria hivyo atakayepatikana atakabiliwa kisheria.

Akizungumza afisini mwake waziri wa afya Francis Gwama amesema atahakikisha wanaotekeleza kitendo hicho wanachukuliwa hatua, huku akisisitiza kwamba serikali ya kaunti iko imara kuhakikisha kila mkwale anapata haki yake kikatiba.

Wakati uo huo amewataka wakaazi kuripoti visa vyovyote vinavyowahujumu wanapotafuta huduma za matibabu, huku akiahidi kuzungumza na wahudumu wa afya ili kuhakikisha kwamba shughuli zinatendeka kwa njia ya usawa.

Haya yanajiri baada ya lalama kutoka kwa wananchi kuhusiana na kuuziwa dawa wanapotembelea vituo vya afya.

By NewsDesk