Walimu na wanafunzi wa Shule mbalimbali za Upili katika Kaunti ya Mombasa wanaendelea kuyasherehekea matokeo bora ya Mtihani wa Kitaifa wa KSCE yaliyotangazwa jana.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Mama Ngina Mwanahamisi Omar amesema kwamba licha ya changamoto ya janga la Korona matokeo hayo ni bora kuliko ya mwaka wa 2019.
Amesema kwamba walimu walijizatiti kukamilisha mtaala kwa wakati vilevile wanafunzi walijisomea zaidi wakiwa nyumbani.
Shule hii ilikuwa na jumla ya Watahiniwa mia moja sabini na watano na robo tatu miongoni mwao walipata gredi itakayowawezesha kujiunga na Vyuo vikuu.
Shule ya upili ya Sheikh Khalifa hapa mjini Mombasa ndio imeibuka bora katika kaunti ya Mombasa kwenye matokeo hayo baada ya mwanafunzi wa kwanza wa shule hio Asia Abubakar kupata grade A ya alama 82.
Miongoni mwa shule zilioandikisha matokeo bora hapa Mombasa, ni shule ya upili ya Light Academy, Shule ya Upili ya Istiqama na shule ya upili ya Qubaa Muslims.
By Reporter Warda Ahmed