HabariSiasa

Wakili tajika George Kithi, ameishtumu vikali serikali ya kitaifa kwa kile anachokidai kuwa haitii sheria.

Wakili tajika ambaye pia amejitokeza kuwania kiti cha useneti kaunti ya kilifi  George Kithi, ameishtumu vikali serikali ya kitaifa kwa kila anachokidai kuwa haitii sheria.

Akizungumza na meza yetu ya habari katika kipindi cha sauti asubuhi, Kithi amesema kuwa serikali ya kitaifa inatumia vibaya mamlaka kwa kupuuza maagizo ya Mahakama kila uchao, jambo ambalo anadai kuwa ni hatari kwa wananchi ambao taifa lao linakiuka sheria kama serikali ya jubilee.

Kithi anasema kuwa kukataa kwa rais Uhuru kenyatta kuteuwa majaji 41 walioteuliwa na tume ya idara ya mahakama JSC, ni moja ya changamoto zinaikumba idara ya mahakama, aidha ameongeza kuwa hatua imewafungia nje majaji wa 3 kutoka ukanda wa Pwani.

By David Otieno