Jaji wa mahakama ya rufaa Daniel Musinga amesema jopo la majaji saba ndilo litasikiza na kuamua kesi za kupinga uamuzi wa mahakama kuu kuhusu mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia ripoti ya BBI.
Jaji Musinga ameyasema haya kwenye kikao ambacho kinaendelea cha majaji wa mahakama ya rufaa na mawakili wa pande husika, kuhusu namna kesi hiyo itakavyoendeshewa
Jaji Musinga aidha anatarajiwa kuteua majaji hao saba ambao watasilikiliza rufaa hiyo ambayo iliwasilishwa na tume ya uchaguzi IEBC, Rais Uhuru Kenyatta, Kinara wa ODM Raila Odinga, Mwanasheria mkuu Paul Kihara.
Ata hivyo mawakili wa pande husika wametaka rufaa hiyo isikizwe mahakamani na wala sio kupitia mfumo wa kidijitali.
By Joyce Mwendwa