Bara la Afrika litapokea angalau dozi milioni 5 za chanjo dhidi ya virusi vya Corona kutoka Marekani hivi karibuni.
Rais Joe Biden ametangaza kuwa nchi ya Marekani inatazamia kupeana misaada ya takriban dozi milioni 80 kote duniani kufikia mwisho wa mwezi wa Juni.
Asilimia 75% ya misaada hiyo ya dozi itasambazwa kupitia mpango wa COVAX huku asilimia 25% ikisambazwa kwa nchi zinazozihitaji sana .
Dozi milioni 19 za chanjo hizo zitasambazwa kote duniani katika awamu ya kwanza kupitia mpango wa Covax huku bara Afrika likipokea takriban dozi milioni 5 ambazo zitapatianwa kwa nchi zitakazochaguliwa na Jumuiya ya Umoja wa Afrika(AU).
Asilimia 2% pekee ya watu katika bara la Afrika ndio wamepokea angalau chanjo moja ya chanjo ya COVID 19 huku asilimia 0.6 pekee wakipokea chanjo zote mbili.
By Hajj Kibwanga