Wizara ya leba imependekeza mpango wa serikali wa kuwasaidia wakongwe, mayatima na walemavu wa inua jamii kutengewa shilingi bilioni 4.7 katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/2022.
Akizungumza katika kaunti ya Baringo waziri wa leba Simon Chelugui, amesema fedha hizo zitanufaisha zaidi ya watu laki moja kujumuishwa kwenye mpango huo utakaohakikisha wanapa marupurupu kila mwezi ili kujisaidia.
Chelugui aidha amedokeza kwamba baraza la mawaziri lilipasisha miswada ambayo itawasilishwa bungeni ili kupitishwa, na pindi tuu itakapotiwa saini na rais Uhuru Kenyatta, basi wakenya zaidi watajumuishwa kwenye mpango huo.
By Warda Ahmed