HabariNewsSiasa

Jaji mkuu Martha Koome amuagiza rais kuwateua majaji sita aliowatenga…..

Jaji mkuu Martha Koome ametoa msimamo wake rasmi kuhusu suala la majaji  sita ambao hawakuteuliwa na rais Uhuru Kenyatta, miongoni mwa majaji 40 waliopendekezwa.

Jaji Koome amemuagiza rais Uhuru Kenyatta, kuwateua majaji wote waliopendekzwa na tume ya JSC bila ya masharti.

Akikariri msimo wake kwamba atahakikisha rais Kenyatta anawaidhinisha majaji sita aliowakataa wakiwemo wawili walioharamisha mchakato wa BBI, Jaji Koome amesema uhuru wa majaji utalindwa huku akimuhimiza rais kuwateua majaji hao waliosalia kwani kuna mirundiko ya kesi ambazo zinasubiri kuamuliwa nao.

Tayari kesi kadhaa zimewasilishwa mahakamani kumshinikiza rais Kenyatta kuwaidhinisha sita hao licha ya kuwakataa bila sababu hasaa kuwekwa wazi.

Kuhusu migogoro iliyopo baina ya serikali tendaji na idara ya mahakama, Koome amesema hatajihusisha na migogoro yenye utata kwani jukumu lake ni kulinda katiba bila ya kushiriki siasa.

By Warda Ahmed