Habari

UAMUZI WA MURUATETU KUTUMIKA TU KWA WALIOHUKUMIWA KIFO

Maelfu ya wafungwa ambao walikuwa wamekuwa wakisubiri kupunguziwa miaka ya vifungo vyao kufuatia kesi dhidi ya Francis Muruatetu wamepata pigo baada ya mahakama kuu kusema kuwa uamuzi wa Muruatetu utatumika tu kwa waliohukumiwa kifo kufuatia mauji na wala si makosa mengine kama uwizi wa kimabavu na ubakaji.

Muruatetu pamoja na watu wengine 6 walihukumiwa kifungo kufuatia mauaji ya mfanyibiashara Lawrence Githinji mnamo Februari mwaka wa 2000

Jaji mkuu Martha Koome akisoma uamuzi ulioafikiwa na majaji wote amesema kwamba uamuzi wa Muruatetu utatekelezwa tu kwa watakaohukumiwa kifo kutokana na kesi za mauaji pekee

Itakumbukwa kuwa mwaka 2017 Muruatetu kupitia wakili wake Fred Ngatia alitaka hukumu hiyo iondolewa kwani katiba ya sasa hairuhusu hukumu ya kifo ambapo walishinda kesi yake huku hukumu dhidi yake ikipunguzwa hadi miaka 30.

 

BY JOYCE MWENDWA