Mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga amekanusha madai yanayohusishwa na viongozi kuhusika katika kisa cha mauaji ya watu wa watatu juma lililopita katika wadi ya Junju eneo bunge la Kilifi Kusini.
Kwa mujibu wa Chonga tukio hilo ni la uhalifu wa kawaida lakini halifai kuhusishwa na maswala ya kesi za mashamba.
Chonga amesema pindi uchunguzi unaofanywa na maafisa wa polisi utakapokamilika chanzo halisi cha mauaji hayo kitabainika.
Chonga hata hivyo amekashifu mauaji hayo huku akiwataka wakazi kutochukua sheria mikono mwao.
Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai kwenye taarifa kwa vyombo vya habari amesema baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaochochea wakazi watachukuliwa hatua za kisheria.
BY ERICKSON KADZEHA