Jopo la tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC hii leo bado linaendelea na zoezi la kusaili makamishna wapya wa tume hiyo katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi.
Mahojiano haya yalianza wiki tatu zilizopita huku Saeed Khamees akiwa mwaniaji wa kwanza kuhojiwa hii leo wengine na watakaohojiwa hii leo ni dtk. Salim Said na Anna Mbii-Kiuluku.
Said ameelezea umuhimu wa maandalizi ya mapema kama moja wapo wa njia za kuepuka tetesi baada ya uchaguzi mkuu kufanyika.
Wawaniaji wa nyadhifa za makamishna ni wakenya 36 waliotuma maombi lakini mmoja wao aliweza kujiondoa.
Aidha, baada ya zoezi hili jopo hili lapania kujaza pengo la makamishna 4 zilizowachwa wazi baada makamishna hao kujiuzulu miaka mitatu iliyopita ikiwemo Roselyne Akombe, Connie Maina, Paul Kurgat na Margrate Mwachanya.
BY CAROLINE NYAKIO