AfyaHabari

KAUNTI YA KILIFI KUWEKA MIKAKATI MIKALI ZAIDI YA KUTHIBITI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA.

Serikali ya kaunti ya Kilifi itaweka mikakati mikali zaidi ya kuthibiti maambukizi ya virusi vya corona juma lijalo baada ya kushuhudiwa ongezeko la visa vya maambukizi siku za hivi karibuni.

Gavana wa kaunti ya Kilifi amesema kamwe hawawezi kuruhusu maafa zaidi yanayosababishwa na homa hiyo kali ya mapafu na kusisitiza tayari mikakati hiyo itaanza kutekelezwa juma lijalo.

Akizungumza huko Dabaso, Kingi amesema kwa muda wa mwezi mmoja pekee kaunti ya Kilifi imepoteza takriban watu sita kutokana na ugonjwa wa corona.

Wakati uohuo Gavana Kingi amewataka wakaazi kaunti hiyo kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona.

Kingi ametahadharisha kuwa endapo wakaazi wataendelea kupuuza masharti hayo,huenda kaunti hiyo ikawa katika hatari zaidi ya kupoteza watu wengi.

 

BY JOSEPH YERI