HabariMazingira

MISITU KUBORESHWA KAUNTI YA KWALE NA WWF.

Shirika la World Wide Fund (WWF) linalenga kuanzisha mpango wa kurekebisha maeneo ya misitu yaliyoharibiwa katika kaunti ya Kwale.

Afisa wa shirika hilo Nathaniel Mwangeka amesema kuwa mpango huo unalenga kuhakikisha kaunti hiyo inaafikia asilimia 10 ya misitu nchini.

Akizungumza katika eneo la Makongeni huko Msambweni, Mwangeka ameeleza kwamba mpango huo utatekelezwa kwa kuishirikisha jamii.

Afisa huyo amedokeza kwamba kaunti ya Kwale iko na asilimia ndogo ya idadi ya misitu ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.

Hata hivyo, Mwangeka amesema kuwa wanashirikiana na wadau mbali mbali ili kuimarisha idadi ya misitu katika kaunti hiyo.

 

BY KWALE CORRESPONDENT