Kamati inayohusika na biashara katika bunge la kitaifa hii leo imezuru ufuo wa bahari Pirates na bustani ya Mamangina kufuatia hoja iliyowasilishwa bungeni na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ya kutaka kufunguliwa kwa maeneo hayo mawili.
Kamati hiyo ikiongozwa na mbunge wa Voi Jones Mlolwa na mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime miongoni mwa wabunge wengine, kwa sasa inawataka washikadau katika serikali ya kaunti ya Mombasa kufika mbele ya kamati hio kuelezea kuhusiana na suala la kuvunjwa kwa vibanda vya biashara katika maeneo hayo mawili sawia na kutaka kufahamu ni mikakati gani wizara ya afya nchini imeweka ili kuona kuwa maeneo hayo mawili yanafunguliwa kikamilifu.
Aidha kamati hio imetoa wiki mbili ya kupatikana kwa suluhu la kudumu pindi tu watakapo kaa kwenye kikao kujadili suala hilo na washikadau katika serikali ya kaunti ya Mombasa pamoja na wadau kutoka wizara ya afya nchini.
Wakati huo huo mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesisitiza haja ya serikali kufungua uchumi kutokana na kile anachosema kuwa kwa sasa wananchi wengi wanaumia,ikiwemo wafanyibiashara wa maeneo hayo mawili.
Vile vile amesisitiza haja ya chanjo kwa wote.
Kim Mariga ni mwenyekiti wa wafanyiashara katika bustani ya mamangina.
Maneo hayo mawili ni miongoni mwa maeneo ya umma nchini yaliyofungwa na serikali kwa kuhofia msambao wa virusi vya corona miongoni mwa wakaazi.
By reporter