HabariNews

Wanafunzi 196 waliofanya KCPE bado hawajajiunga na shule za upili katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini…

Wanafunzi 196 waliofanya mtihani wao wa darasa la nane KCPE bado hawajajiunga na shule za upili katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini.

Kulingana na naibu kamishena wa eneo bunge la Kilifi kaskazini Josphat Mutisya ni kuwa hadi kufikia sasa asilimia 99.02 ya wanafunzi waliofanya mitihani yao ya darasa la nane wamefanikiwa kujiunga na shule za upili kaunti ya Kilifi.

Amesema maeneo bunge ya Kilifi Kusini na Malindi yanaongoza kwa idadi ya wanafunzi waliojiunga na shule za upili hatua hii ikiwa ni kutokana na mpango wa kuhahakisha kuwa asilimia 100 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa KCPE wanajiunga na shule za upili.

Kwa upande wao wazazi wanasema hali ngumu ya uchumi imechangia kuwachelewesha watoto wao kujiunga na shule za upili huku wakizitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kuwagharamia watoto ambao hawajajiunga na shule za upili.

BY NEWS DESK