HabariNews

Wanafunzi kutoka shule za vijijini waibuka washindi katika mashindano ya kitaifa ya uandishi Insha 

Wanafunzi kutoka shule za vijijini wameibuka washindi katika mashindano ya kuandika insha  ambapo wanafunzi 23,000 kutoka shule za umma 11,300 walihusika katika mashindano hayo.

Mwongeli Mulwa kutoka Makueni, Denise Nguhi (Machakos), Mitchele Rono (Elgeyo Marakwet), Melvin Koech (Elgeyo Marakwet) na Emmanuel Okinyi (Migori) wamekuwa wanafunzi watano bora katika mashindano hayo.

Washindi hao wametuzwa katika tamasha iliyoandaliwa kaunti ya Kilifi ambapo waziri wa elimu prof George Magoha, waziri wa utalii  najib Balala ,walimu pamoja na washikadau kutoka chama cha  wa walimu wakuu nchini KEPSHA.

Shindano hilo lilidhaminiwa na kampuni ya Pwani Oil kwa ushirikiano na wizara ya elimu na chama cha walimu wakuu wa shule ya msingi KEPSHA.

Akizungumza wakati wa kuwatuza wanafunzi hao waliofanya bora mkurugenzi wa mauzo Rajul Malde amesema kuwa nia ya kuandaa shindano kama hilo ni kumpatia nafasi mwanafunzi ya kueneza ujuzi wake akiwa bado mdogo.

Kwa upande wake waziri wa elimu prof George Magoha ameeleza kutobabaishwa na hatua ya baadhi ya wakenya ambao wamewasilisha kesi mahakamani kupinga mtaala wa umilisi CBC.

Magoha amesema kamwe hatokubali kusitishwa kwa mfumo huo wa Elimu, akiongeza kuwa wanaopinga utekelezaji wake hawana ufahamu wowote kuhusu umuhimu wake.

“Mimi nikama fullback katika mchezo wa mpira,kazi ya fullback nikuzuia kutofungwa mabao na nitafanya hivyo katika wizara ya elimu, waniwache nifanye kazi yangu. Waniepele Kortini tutapatana nao huko nab ado tutatetea mfumo wa cbc kwa manufaa ya watoto wetu na elimu bora kwa faida ya maisha yao ya baadae.” Alisema Magoha.

https://www.facebook.com/sautiyapwanifm/videos/214058910712874

Aidha Magoha amepongeza shule za pwani kwa kuongoza katika utekelezaji bora wa mtaala huo.