Huenda ikawa afueni kwa madereva wa masafa marefu kutoka kaunti ya Mombasa kuendelea na safari zao za kibiashara katika taifa la Sudan Kusini bila tashwishi yoyote.
Hii ni kufuatia mkutano uliofanyika na wajumbe kutoka kaunti ya Mombasa wakiongozwa na gavana wa kaunti hii Ali Hassan Joho walipokutana na rais wa taifa la Sudan Kusini kujadiliana afueni ya madereva hao mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake baada ya kufanya mkutano wa faragha na baadhi ya washikadau mbunge wa Jomvu Badi Twalib amesema kuwa kupitia mazungumzo hayo rais wa Sudan Kusini Salva Kiir aliwahakikishia madereva hao usalama wao wanaposafiri nje na ndani ya taifa lake kutekeleza biashara.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitaifa wa maswala ya kiuchumi na viwanda KNCCI Mustafa Ramadhan amesema kuwa wanatarajia kuweka mkataba wa maelewano kati ya mataifa hayo mawili kwa ajili ya kuweka msingi imara wa kutekeleza biashara.
BY NEWS DESK