Maelfu ya wafuasi wa rais Adama Barrow wamemiminika mitaani kusherehekea ushindi wa rais huyo wa Gambia kwa kipindi cha pili mfululizo baada ya matokeo rasmi kutangazwa hii Jumatatu.
Barrow ambaye ushindi wake katika uchaguzi wa rais miaka mitano iliyopita ulimaliza miongo miwili ya utawala wa kidikteta wa rais wa zamani wa taifa hilo Yahya Jammeh ameshinda kipindi cha pili cha uchaguzi wa rais kwa kupata zaidi ya silimia 53 ya kura.
Mpinzani wake wa karibu Ousainou Darboe amepata asilimia 28 ya kura kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi.
Mkuu wa hiyo, Alieu Mommar Njai amemtangaza Rais Barrow kuwa mshindi wa uchaguzi huo mbele ya waandishi wa habari masaa machache baada ya wagombea wa upinzani kulalamikia matokeo hayo hasa baada ya kutangazwa kwamba Barrow alikuwa anaongoza matokeo ya awali ya uchaguzi huo.
BY NEWSDESK