Huku serikali ikizidi kutoa wito kwa wakenya kujitokeza na kupata chanjo dhidi ya maradhi ya covid 19, baadhi ya wakenya wanaonekana kususia chanjo hiyo kutokana na kasumba potuvu zinazohusishwa na chanjo hiyo.
Kulingana na Joseph Kenga afisa wa chanjo katika hospitali ya rufaa ya Coast General hapa jijini Mombasa, ni kuwa baadhi ya watu wanapopokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona, huenda wakahisi hali isiyo ya kaiwada jambo ambalo analitaja kuwa la kawaida.
Kenga aidha anasema kuwa ili kuepuka kuhisi hali hiyo ni vyema mtu kupumzika kwa takriban masaa 4 baada ya kupokea chanjo ya Covid-19.
Akiendelea kuwahimiza wakenya kujitokeza ili kupokea chanjo dhidi ya Covid-19, Kenga amewahimiza wananchi kunywa maji ya kutosha ili kuuwezesha mwili kupata nguvu baada ya kupokea chanjo
Baadhi ya wakenya wangali kupokea chanjo ya Covid-19, kutokana na taarifa za kupotesha zinazosambazwa kwenye mitando ya kijamii.
BY NEWS DESK