Shule ya kibinafsi kote Nchini zinaendelea na mikakati ya kujenga madarasa ya ziada ili kukidhi mahitaji ya mfumo wa elimu ya umilisi wa CBC.
Shule za msingi zitapunguziwa madarasa mawili, saba na nane ili kuendana na mfumo wa CBC ambao unaanzia gredi ya kwanza hadi ya sita.
Baadhi ya wamiliki wa shule za kibinafsi tayari wameanza kubadili majengo ya madarasa hayo kuwa madarasa ya sekondari ya msingi yaani Junior Secondary School.
Itakumbukwa kwamba humu Nchini, kuna takriban shule elfu 11 ambazo ni za msingi huku zile za upili zikiwa elfu 1 na 600 pekee.
Haya yanajiri huku Wizara ya Elimu ikiwashauri wamiliki wa shule hizo kujenga madarasa ya Sekondari ili kurahisisha utekelezaji wa CBC ambao ulianza rasmi mwaka 2017 kwa madarasa ya gredi ya kwanza, na kufikia mwaka huu CBC imetekelezwa hadi gredi ya tano ambapo utekelezaji huo umeratibiwa kwenda hadi gredi ya 12 ifikapo mwaka 2028.
BY NEWSDESK