AfyaHabariLifestyleNews

Lazima uwe umechanjwa ili upate huduma za umma;, yatangaza serikali

Serikali kupitia Wizara ya Afya, sasa imetangaza hatua kali zaidi kwa watu ambao hawajachanjwa virusi vya corona huku maambukizi ya COVID-19 nchini yakiongezeka maradufu.
Akizungumza na vyombo vya habari,Katibu mwanamizi wa Afya (CAS) Dkt. Mercy Mwangangi, amesema kuwa kuanzia sasa, kila mtu anayetafuta huduma za serikali anastahili kuwa amechanjwa mara 2 na kuonyesha uthibitisho wa chanjo hiyo katika nakala au muundo wa dijiti.
Mwangangi amesema uthibitisho huo utahitajika katika maeneo ya umma, mahoteli ,mbuga za wanyama, baa, mikahawa, na pia katika njia za usafiri wa umma miongoni mwao safari za ndani, treni na matatu.
Mwangangi amesema wageni, watalii na wasafiri wote kutoka mataifa ya nje lazima wapatiwe chanjo kamili na kutoa uthibitisho kabla ya kuingia nchini.