Rais Uhuru Kenyatta amedokeza kuwa serikali ya Hungary imetoa dola milioni 50 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 5.6 ambazo zitaekezwa katika sekta ya afya, elimu, kilimo pamoja maji na usafi.
Kenyatta amesema kuwa ziara ya rais HUYO ITAyapa mataifa haya mawili nafasi ya kuimarisha uhusiano ambao umekuwepo kwa miaka 5.
Kwa upande wake rais Ader ni kwamba taifa liko tayari kuiunga mkono Kenya katika lengo lake la kuongeza idadi ya misitu kwa aslimia 10 kupitia kuwapa waandisi waliobobea katika masuala ya misitu.
Rais Ader vilevile amesema kwamba kutokana na kuimarika kwa kiwango cha maisha ulimwenguni, kumechangia katika uchafuzi wa mazingira na kuwa wako tayari kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa njia za kisasa.