Licha ya sheria ya usawa wa kijinsia katika bunge la kitaifa kuwa kwenye katiba ya nchi, Serikali chini ya uongozi wa raisi uhuru Kenyatta imeshindwa kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa kikamilifu.
Kwa mujibu wa mtaaalamu wa masuala ya kijinsia Cesil Maundu, ni kwamba licha ya raisi uhuru Kenyatta kuwa na jukumu la kuhakikisha sheria hiyo inafuatwa, amekosa kuchukuwa hatua mwafaka za kufanikisha utekelezwaji wa sheria hiyo.
Maundu hata hivyo, amewataka wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya hapa nchini hususan katika ukanda wa pwani kujitosa kwenye ulingo wa siasa kuwania nyadhifa za uongozi akisema kwamba ndio suluhu la mzozo huo.
Aidha, mtaalamu huyo amewakosoa wanawake wanaotegemea uteuzi kuingia katika mabunge ya hapa nchini, huku akiwataka watupilie mbali dhana zilizopitwa na wakati za uongozi kuachiwa wanaume.
Kauli yake inajiri huku wanawake mbalimbali katika ukanda wa pwani wakijizatiti kujitosa kwenye siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa agosti 9 mwaka huu.