HabariMombasaNewsUncategorized

Wanafunzi 6 wafanya mtihani wa KCSE wakiwa Gerezani kaunti ya Kwale.

Watahiniwa 6 kaunti ya Kwale watalazimika kufanya mtihani wa KCSE gerezani baada ya kudaiwa kuhusika na uchomaji shule mwaka jana.
Akizungumza na wanahabari baada a kufunguliwa kwa kasha la mtihani mkurugenzi wa elimu kaunti ya Kwale Martin Cheruiyot amesema tayari wanafunzi hao wamepokea ushauri nasaha ili kuhakikisha wanafanya mtihani huo vyema.
Cheruiyot amesisitiza kuwa idara elimu kaunti hio kwa ushirikiano na idara ya usalama, imeweka mikakati ya kutosha kuhakiksha kuna usalama wa watahiniwa sawia na magari ya kutosha ili kufanikisha usafirishaji mtihani huo.