HabariMazingiraNews

Wataalamu wa kilimo wameishauri serikali ya kaunti ya Kilifi kubuni mbinu mwafaka za kuhifadhi maji.

Wataalamu wa kilimo wameishauri serikali ya kaunti ya Kilifi kubuni mbinu mwafaka za kuhifadhi maji hususan wakati huu ambapo mvua zisizotabirika hunyesha kwa ajili ya kufufua kilimo ambacho kwa sasa kimeonekana kufifia.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa kilimo eneo bunge la Rabai katika kaunti ya kilifi John Mbaji, ni kwamba miaka ya hivi karibuni mvua imekuwa changamoto kupatikana hususan katika mkoa wa pwani kutokana na mabadiliko ya hali ya anga.
Mtaalamu huyo ametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo ikishirikiana na wizara ya kilimo kuhakisha maji ya mvua inayopatikana yanavunwa huku akiitaja kaunti hiyo kuwa tajiri kwa idadi ya mito inayopatikana hali anayosema endapo serikali ya kaunti itatilia maanani kilimo kitaimarika tena.
Kuhusu suala mavuno kupatikana kwa wingi kama ilivyokuwa awali, mtaalamu huyo anakiri kwamba ni vigumu kutokana kukosekana kwa rotuba muhimu katika ardhi za wakulima.
Hata hivyo , Mbaji amesisitiza utumizi wa pembejeo mwafaka ikiwemo kutumia mbolea bora pamoja na kupanda aina ya mimea ikiwemo baadhi ya mbegu za mahindi zisizohitaji mvua nyingi kutoa mazao akiitaja kuwa suluhu kwa ukosefu wa chakula.