AfyaHabariNews

BODI YA USIMAMIZI YA KMTC YATAKIWA KUTOA MUONGOZO.

Waziri wa afya Mutahi kagwe ameamuru bodi ya usimamizi wa chuo cha mafunzo ya udaktari nchini KMTC kutoa muongozo wa ni vipi wahudumu wa afya watapata fursa ya kutoa huduma katika nchi za ugaibuni.
Akizungumza katika hoteli moja mjini Malindi Kagwe ameamuru bodi hiyo kuanzisha mpangilio ambapo wahudumu hao watafahamishwa kuhusu masuala ya nchi hizo.
Ameamuru bodi hiyo kutoa mpangilio wa nivipi wataalamu wa afya hawatakosa nafasi za ajira katika nchi zengine.
Wakati uohuo afisa mkuu wa afya ya Umma Dkt Patrick Amoth amesema kuna haja ya wahudumu wote nchini kupata mafunzo maalum ya kutumia teknologia ya kisasa.
Amoth anasema nchi nyingi ulimwenguni taari zimekumbatia teknologia ya kisasa akitoa changamoto kwa wahudumu wa afya humu nchini kujitokeza endapo mpango huo utaanzishwa.
Wawili hao wameyasema haya baada ya kuzindua sera ya kuwakinga wauguzi dhidi ya kuandamwa kisheria ikiwa wamefanya makosa wakiwa kazini.

BY EDITORIAL DESK