Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uspika kwenye bunge la kitaifa.
Kalonzo ambaye amejiondoa kufuatia ushauri wa baraza kuu la chama cha Wiper, haijawekwa wazi iwapo atawania wadhfa huo katika seneti au la.
Hata hivyo kujiondoa kwa Kalonzo kunamuacha Kenneth Marende kuwa pendekezo la Azimio akitarajiwa kumenyana na seneta wa Bungoma Moses Wetangula.
Wakati huo huo aliyekuwa akiwania kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya chama cha UDA Hassan Sarai amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwa spika wa Seneti.
Kupitia ujumbe katika mtandao wake wa Facebook, Sarai amesema uamuzi huu umeafikiwa baada ya kikao na raisi mteule William Ruto na kuwaomba wafuasi wa mrengo wa Kenya Kwanza kumuunga mkono aliyekuwa gavana wa Kilifi Amason Kingi.
BY EDITORIAL DESK