Wakulima pamoja na wakaazi wa kaunti ya Kwale wameombwa kupanda miti kwa wingi ili kuzuia mmomonyoko wa udongo kwenye mashamba yao kama njia ya kurudisha hadhi ya ardhi zao walizokuwa wakizitumia kwa kilimo miaka ya awali.
Akizungumza huko Diani kaunti ya Kwale wakati wa uzinduzi wa mradi wa upandaji miti mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kuhifadhi mazingira la Restore Africa Jonathan Muriuki amedokeza kuwa mradi huo unafanya kazi katika nchi sita katika bara afrika unaotarajiwa kuchukua muda wa miaka mitano.
Aidha Muriuki ameongeza kusema kuwa mradi huo unatarajiwa kufikia Wakulima laki mbili na nusu na kupanda miti kwenye hekari laki 2.5 ndani ya kaunti za Kwale, Tana River, Narok na Elgeyo- marakwet.
Hapa kaunti ya Kwale mradi huo utafanyika katika baadhi ya kaya na sehemu kame.
Wakati uo huo asema kuwa mabadiliko ya hali ya anga yamechangia pakubwa uharibifu wa hali ya anga na kupelekea kuharibu rotuba ya ardhi, hivyo ipo haja ya wakaazi kushiriki zoezi la upandaji miti ili kuzuia kusambaa kwa hewa isio salama kwa afya za wakaazi.
BY EDITORIAL TEAM