HabariNews

Onyo Kali latolewa na serikali ya kaunti ya kwale kwa wanaoendeleza uharibifu wa mabomba ya maji.

Onyo Kali latolewa na serikali ya kaunti ya kwale kwa wanaoendeleza uharibifu wa mabomba ya maji na kujiunganishia wenyewe kinyume na Sheria kwamba Sheria itachukua nafasi yake.

Haya ni kwa mujib wa gavana wa kaunti ya kwale Fatuma Achani amesema kumeshuhudiwa ongezeko la visa hivyo vya ukataji wa mabomba ya maji kiholela hali iliyopelekea uhaba wa maji katika baadhi ya sehemu mbali mbali za kaunti hiyo.
Achani amesema Hatua hizo zitahakikisha wakaazi wa kwale wananufaika na huduma bora za maji huku akiwarai waakazi kulinda raslimali za kaunti.

Kwa upande wake kamishna wa kaunti hiyo Gideon Oyagi amewataka wakaazi kuripoti visa hivyo kwa maafisa wa usalama ili washukiwa wachukuliwe Hatua Kali za kisheria.

BY EDITORIAL DESK