FoodHabariNews

Kamati ya kupambana na ukame kaunti ya Kwale imeweka mikakati ya kuzuia visa vya wizi wa chakula cha msaada.

Naibu kamishna wa Matuga kaunti ya Kwale Lucy Ndemo amesema kuwa kamati ya kupambana na ukame kaunti hiyo imeweka mikakati ya kuzuia visa vya wizi wa chakula cha msaada katika eneo hilo.

Ndemo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo katika eneo bunge la Matuga, ametoa onyo kali kwa wahusika kwamba watakabiliwa kisheria.

Akizungumza baada ya kupokea chakula hicho kutoka serikali ya kitaifa mjini Kwale, Ndemo amesema kuwa kamati hiyo iko macho kukabiliana na visa hivyo.

Wakati uo huo, Ndemo amedokeza kwamba chakula hicho kitatolewa kwa wanafunzi wanaokubwa na baa la njaa katika shule za kutwaa na maalum.

Jumla ya magunia 400 ya mchele, 160 ya maharagwe na katoni 100 za nyama ya mikebe zitapelekwa kwa wakaazi walioathirika na ukame katika maeneo ya Mbuguni, Mwachome, Msalani na Mazumalume.

BY EDITORIAL DESK