Watahiniwa wa mwaka huu pamoja na wanafuzi wa shule zenye mahitaji maalum wataweza kupata chakula cha msaada wakati wa mitihani ya kitaifa ndani ya kaunti ya Kwale.
Hii ni kauli ya gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani baada akiagiza kamati ya kukabiliana na ukame na majanga kwale kusambazia chakula shule za kutwa na Maalumu huku wakijiandaa kufanya mitihani ya kitaifa mwezi Disemba.
Ni Kauli iliyoungwa mkono na kaunti kamishna wa kwale Gideon Oyagi akisema kuwa Serikali ya kitaifa na kuanti itashirikiana ili kukabiliana na ukame Kwale.
Wakati uo huo kiongozi huyo amewataka wazee, watu wanaoishi na mahitaji maalum sawia na mayatima kuweza kuhesabiwa kupata chakula hicho.
BY EDITORIAL DESK.