HabariNews

Uchawi kutoka eneo bunge la Kinango na viunga vyake umetajwa kutatiza hali za usalama maeneo hayo.

Tuhuma za uchawi kutoka eneo bunge la Kinango na viunga vyake zimetajwa kutatiza hali za usalama maeneo hayo hususan usalama wa wazee.

Kulingana na msaidizi wa kamishna eneo la Kinango Francis Gichohi amelaani vikali kitendo cha wazee kuuwawa kwa tuhuma za uchawi ilhali vijana wamekataa kujituma kujitafutia maisha badala yake wanajihusisha na mauwaji ya wazee ili warithi mali na ardhi zao.

Gachohi amewataka wakaazi kukomesha tabia hiyo kwani ni kinyume na sheria ikizingatiwa kwamba kila mtu ana haki ya kuishi.

Aidha amewarai wakaazi wa eneo bunge hilo kudumisha amani.

Haya yanajiri huku visa vya kuuliwa kwa wazee vikionekana kuchipuka tena ambapo kisa cha hivi majuzi kikiripotiwa eneo la Lutsangani.

BY EDITORIAL TEAM