Wakaazi wa eneo la Kaya bombo na Kiteje kaunti ya Kwale wanalalamikia ongezeko la visa vya utovu wa usalama katika eneo hilo .
Wakiongozwa na Bechari Mwandegwa, wanasema kuwa magenge ya kihalifu yanayojificha katika msitu wa kaya bombo hutumia kifaa maalumu cha kiteknologia kuwapoteza fahamuni wenyeji kabla ya kuwapora mali zao.
Sasa wanaitaka idara ya polisi kuanzisha oparesheni katika msitu huo na kuyakabili magenge hayo ili wenyeji waishi kwa usalama.
Kwa upande wake OCS wa kituo cha polisi cha Kwale Philip Ngatia amethibitisha kudorora kwa usalama katika eneo hilo japo kusema kwamba idara ya polisi inajizatiti kukabiliana na magenge yanayotekeleza wizi wa kimabavu katika eneo hilo.
BY EDITORIAL DESK