HabariNews

Umaskini watajwa kuwa chanzo kikuu cha ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia.

Umaskini ndio chanzo kikuu cha ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia hususan wakati huu ambapo baadhi ya sehemu zimekubwa na kiangazi katika kaunti ya Kwale.

Kulingana na afisaa wa shirika la kibinafsi linalo pambana na dhulma za kijinsia katika jamii la Haki Yetu Munira Abubakar amedokeza kuwa sababu kuu ya mizozo katika jamii ni hali duni za kiuchumi iliyochangiwa na mabadiliko tabia-nchi ambapo wasichana wengi wamejitia katika ngono biashara kufuatia ukosefu wa mahitaji muhimu kwenye familia.

Aidha Abubakar ameendelea kusema kuwa mbali na baadhi ya wasichana kubeba uja-uzito wengine hukimbilia kuolewa jambo linaloongeza idadi ya ndoa za mapema kutokana na umaskini uliopo kwenye familia zao.

Aidha afisaa huyo amewataka wasichana kutoka sehemu zilizoathirika na ukame kutotumia changamoto kama kizingiti cha kutofikia ndoto zao za maisha badala wazichukue kama ngati ya kufika wanapotaka katika kufanikisha maisha yao badae.

BY EDITORIAL DESK